Haki ikikosa katika jamii yeyote kunakuwepo na mafarakano. Hii ni kwa sababu kuna wanaoumia na wengine wanafurahia. Nchi yeyote kusipokuwepo na haki, amani haipo na kama ipo ni ya muda na kutoweka kwake ni hakika.
Mfano mzuri ni tofauti iliyopo katika mishahara ya watumishi wa umma katika nchi maskini. Unakuta mshahara wa chini ni Tsh 150,000/= na mshahara wa juu ni milion 10. Hii maana yake ni kwamba mtu wa mshahara wa juu anamzidi mtu wa mshahara wa chini mara 67. Lakini katika nchi zilizoendelea zingine mtu wa mshahara mkubwa anamzidi wa mshahara mdogo mara 2, 3 au 4 tu. Maana yake Professor anamzidi mfagiaji wa ofisi yake mshahara mara tatu tu, au mwalimu anazidiwa na waziri au katibu mkuu mara nne tu. Katika nchi zisizo na Haki ni kinyume kabisa.
Wakulima wananyonywa kwa kuuza mazao yao kwa bei ya kutupa, huku watoto wao wakisoma na kutibiwa katika mazingira magumu. Nchi zenye Haki kuna ruzuku inatolewa kwa wakulima, mfano akiuza gunia la mahindi 18,000 serikali inamuongezea 18,000 jumla 36,000 pia inampatia pembejeo za kutosha. Shule, afya na maji wanapatiwa kwa uhakika.
Hayo yote hupunguza tofauti iliyopo kati ya walichonacho na wasiokuanacho. Ila kama haki haipo, wasionacho hudai kwa nguvu hivyo kusababisha migogoro na migongano.
Karibuni wadau kwa mjadara.
asante
ReplyDelete